Header Ads

MAREKANI YAKATAA MADAI YA KUISAIDIA IS NCHINI SYRIA

Marekani imetaja madai ya rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan kwamba inasaidia wapiganaji wa, kuwa ya upuuzi.

Msemaji wa serikali Mark Toner amesema madai hayo hayakuwa na msingi.
Kiongozi wa Urusi alisema kuwa ana ithibati tosha iliyoonyesha Marekani imetoa msaada kwa makundi ya Kikurdi ya YPG na PYD. Wanajeshi wa Uturuki wamekuwa wakipigana kuiondoa IS kutoka Kaskazini mwa Syria.
"Wamekuwa wakitushtumu tunaisaidia Daesh," bwana Erdogan alisema kwenye kikao cha waandishi wa habari mjini Ankara, akitumia jina mbadala la IS.
"Sasa wanayasaidia makundi ya kigaidi yakiwemo Daesh, YPG, na PYD. "Ni wazi kabisa, Tuna ithibati tosha iliyothibitishwa, pamoja na picha na hata video."

No comments

Powered by Blogger.