Header Ads

Kosa lililomfanya YAYA TOURE kufungiwa kuendesha gari Miezi 18 England

MICHEZO Kosa lililomfanya Yaya Toure afungiwe miezi 18 kuendesha gari England  
onDecember 13, 

Kiungo wa kimataifa wa Ivory Coast anayeichezea Man City ya England Yaya Toure leo December 13 2016 jina lake limerudi tena kwenye headlines baada ya kutolewa taarifa kuwa amefungiwa miezi 18 kuendesha gari England.

Toure amefungiwa miezi 18 kuendesha gari na kupigwa faini ya pound 54,000 ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 140 kwa kosa la kuendesha gari akidaiwa alikuwa kalewa, Toure alifika mahakama ya Barkingside Magistrates East London.

Wengi wanashangazwa na tuhuma hizo za Yaya Toure kudaiwa kunywa pombe, Toure aliwahi kukataa zawadi ya mchezaji bora wa mechi ambayo ilikuwa ni shampeni, kwa madai kuwa hawezi kuchukua shampeni kwa sababu ni kinyume na maadili ya dini yake ya kiislamu.

No comments

Powered by Blogger.